Advertisement Live Chat Join Whatsapp
logo Hello!!
You are Welcome
Professional IT Team and Talented Designers * We Fix, We Advice and We Train You
CLOSE ADS
CLOSE ADS

Ufadhili Kupitia Samia Scholarship Kwa Wahitimu Wenye Ufaulu Wa Juu Katika Mitihani Ya Kidato Cha Sita 2022 Katika Tahasusi Za Sayansi


1.0  UTANGULIZI

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanzisha programu ya Ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP.  Ufadhili huu ni mpya hapa nchini kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Tahasusi za Sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN). 

SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa asilimia mia moja (100%) masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi hao ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba.

2.0  SIFA ZA KUPATA UFADHILI

Ufadhili huu utatolewa kwa wahitimu wa kidato cha sita  wenye sifa zifuatazo:

  1. Awe Mtanzania;
  2. Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka 2022 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi;
  3. Awe amepata udahili katika programu za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati au Tiba katika Chuo Kikuu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali ambazo zimetajwa katika kundi la kwanza (Cluster 1) katika Mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2022/2023 unaopatikana kupitia heslb.go,tz
  4. Awe ameomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa;

3.0   MAENEO YA UFADHILI

Ufadhili utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kugharamia maeneo yafuatayo:

  1. Ada ya Mafunzo
  2. Posho ya chakula na malazi
  3. Posho ya Vitabu na Viandikwa
  4. Mahitaji Maalum ya Vitivo
  5. Mafunzo kwa Vitendo
  6. Utafiti
  7. Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu
  8. Bima ya Afya

4.0   MUDA WA UFADHILI

Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharamiwa kati ya miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.

5.0   UTARATIBU WA KUOMBA UFADHILI

Maombi ya Samia Scholarship yatawasilishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kwa siku 14 kuanzia Septemba 28, 2022.

6.0   WAJIBU/MASHARTI YA UFADHILI

Mwanafunzi atakaepata ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP atawajibika kuzingatia masharti yafuatayo:

  • Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ufadhili wa Masomo kati yake na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
  • Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwa ajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja.
  • Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila barua ya idhini ya maandishi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
  • Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya, na kuthibitishwa na chuo husika;
  • Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili kabla ya kuanza masomo, atapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwenda kwa:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Mji wa Serikali Eneo la Mtumba Mtaa wa Afya,
S.L.P 10,
40479 DODOMA, TANZANIA.
Barua pepe: ps@moe.go.tz
  • Iwapo kiwango cha ufaulu wa mnufaika kitashuka chini ya GPA 3.8 katika mwaka wa masomo, ufadhili utasitishwa;
  • Mnufaika anapaswa kujisajili katika Mfumo wa Usimamizi wa Wanafunzi (Students Management System) unaopatikana kupitia https://scholarships.moe.go.tz/

MUHIMU KUZINGATIA:

  1. Ufadhili huu ni wa asilimia mia moja ambao kikomo chake kitazingatia miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
  2. Orodha ya majina ya wanafunzi husika inapatikana kupitia www.moe.go.tz na www.heslb.go.tz
  3. Alama za ufaulu: 3-5 (ME), 3-6 (KE) na 5-9 (wenye mahitaji maalum)

Post a Comment

Previous Post Next Post